MKUU wa jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro ametoa rai kwa wazazi na walimu wilayani Kibiti na Rufiji, kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola juu ya kutoweka kwa wanafunzi zaidi ya 1,300 wakati wa matukio ya kiuhalifu yaliyotokea katika wilaya hizo.
IGP, Sirro ameyasema hayo wilayani Kibaha, mkoani Pwani, katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo ambapo alizungumza na viongozi wa mashirika ya umma, wazee maarufu, wastaafu mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapo.
Amewataka wazazi husika na walimu wa shule za msingi na sekondari ambazo wanafunzi walikuwa ni watoro ama hawajaripoti shule kwa miezi kadhaa kutoa taarifa kwani wapo baadhi ya watoto wanaotumika kufundishwa uhalifu hata wakutumia silaha na watu wasiowema.
Ameeleza amepatiwa taarifa ya wanafunzi zaidi ya 1,300 mkoani hapo ni watoro na hawajulikani walipo hivyo wazazi washirikiane kusaidia jeshi la polisi kujua walipo.
“Kuna baadhi misikiti, makanisa yanadaiwa yanayotumia watoto hawa katika masuala ya kiuhalifu hivyo kuna kila sababu ya kuingia ndani kutafuta suluhu", Amesema Sirro.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
 
Top